Mwimbaji nyota wa muziki toka nchini Nigeria, simi ambaye bado anaendelea kufanya vizuri na album yake mpya na ya tano iitwayo “To Be Honest” yenye mwezi mmoja tangu itoke, amejiunga rasmi na Golden Club ya Boomplay.
Hatua hiyo kubwa kwa Simi inakuja baada ya streams zake zote za Boomplay kufika Milioni 100+ (100,000,000). Simi anakuwa msanii wa kwanza mwanamke kugonga streams hizo.
Aidha, simi anajiunga na wasanii wengine wanaotesa katika anga la muziki kutoka Nigeria, ambao pia tayari wamefikisha idadi ya streams Milioni 100+ katika Boomplay, kama vile Davido, Wizkid, Burna Boy, Fireboy DML, Omah Lay, na Joeboy.