Msanii nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Simi, ametangaza kuachia album yake mpya mwezi ujao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Simi amethibitisha hilo akitoa maelezo kuwa album yake hiyo itaingia sokoni Juni 3 mwaka huu wa 2022.
“Kiukweli kabisa album itatoka tarehe 3 mwezi wa 6”. Ameandika kwenye Instagram yake.
Hii inaenda kuwa album ya tano kwa Simi baada ya album yake ya “Restless II” iliyotoka mwaka 2020.
Album zake nyingine ni pamoja na “Chemistry” ya mwaka wa 2016, “Simisola” ya mwaka wa 2017 na “Omo Charlie Champagne” ya mwaka wa 2019.