Msanii aliyegeukia ukasisi Linet Minyaki maarufu Size 8 amefunguka kuhusu afya yake na kudai kuwa hayuko tayari kupata mtoto.
Katika mahojiano na Nicholas Kioko, kasisi huyo alimtakia Wahu heri katika safari yake ya uja uzito na kudai kuwa hayuko tayari kupata mtoto ila anataka kumfanyia mungu kazi.
Size 8 amefunguka kwa kusema shinikizo ya damu imekuwa ikimsumbua kwa muda jambo ambalo lilimpelekea karibu apotezee uja uzito wake.
Ameenda mbali zaidi na kusema kwamba karibu apoteze maisha yake alipojifungua mtoto wake kwani alipooza upande mmoja wa mabega yake.
Kasisi huyo amesema anapenda watoto na anatamani angeweza kupata watoto kumi lakini kwa sababu ya matatizo ya Afya yanayomsibu ameshauriwa achukue mapumziko.