Msanii wa nyimbo za injili Size 8 Reborn amethibitisha kwamba ni kweli aliondoka nyumbani kwake baada ya kuingia kwenye ugomvi na mume wake DJ MO.
Akizungumza na mashabiki zake mapema leo kupitia channel yake ya Youtube amesema alikuwa amemkasirikia mume wake ambaye alikuwa amemkosoa hivyo alihitaji nafasi ya kukaa pekee yake na kujifikiria.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mateke” amesema anashukuru Mungu wamerudiana pamoja baada kumaliza tofauti zao walipopatanishwa na marafiki pamoja na viongozi wa dini.
Katika hatua nyingine msanii huyo ambaye pia ni kasisi ametoa angalizo kwa mashabiki zake kutoharibu ndoa zao kisa migogoro isiyokuwa na msingi huku akiwataka kutafuta ushauri nasaha mahusiano yao yanapoingiwa na ukungu.
Utakumbuka wikiendi hii iliyopita taarifa za Size 8 kuikimbia ndoa yake ziligonga vichwa vya habari ambapo alidaiwa kuondoka nyumbani kwake akiwa na watoto wake wawili baada ya mume wake DJ MO kumsaliti.