You are currently viewing SIZE 8 ATAWAZWA RASMI KUWA KASISI

SIZE 8 ATAWAZWA RASMI KUWA KASISI

Sasa ni rasmi msanii nyimbo za injili nchini Size 8 ametawazwa kuwa mhubiri baada ya kukabidhiwa cheti rasmi ya kuhudumu kama mtumishi wa Mungu.

Taarifa hiyo imethibitisha na Size 8 mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare baadhi ya picha ya kutawazwa kwake kuwa mhubiri,  hafla ambayo iliongozwa na kasisi Kelvin Ephraim na Jackie Kelvin katika kanisa la JCC, Nairobi.

Hitmaker huyo wa “Mateke” ameelezea namna watu walitilia shaka imani yake kipindi anatangaza kukumbatia ukristo lakini mwisho wa siku anashukuru Mungu amefanikisha ndoto aliyokuwa nayo maishani.

Size 8 amewashukuru wanafamilia na marafiki kwa kusimama nae kwa safari yake ya kutaka kuwa mhubiri wa neno la Mungu kwa kusema kwamba hajakuwa rahisi.

Hata hivyo mashabiki na baadhi ya mastaa wamempongeza kwa hatua hiyo kubwa ambayo amepiga maisha wakimtaka kila la heri kwenye harakati zake za kusambaza injili.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke