You are currently viewing SIZE 8 AWAPA SOMO MASHABIKI ZAKE

SIZE 8 AWAPA SOMO MASHABIKI ZAKE

Msanii wa nyimbo za injili nchini Size 8 amewapa somo mashabiki zake kuwa maisha ni zaidi ya pesa, utajiri na umaarufu kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia instastory yake Size 8 amesema mali ya dunia sio ufunnguo wa furaha maishani bali ni utumwa ambao umewakosesha wengi amani ambapo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa watu wanapaswa kuukimbilia ufalme wa mungu kwani ndio njia pekee ya kupata furaha milele.

Post hiyo ya Size 8 imezua gumzo mtandaoni miongoni mwa mashabiki wengi wakionekana kumuunga mkono kwa kauli yake hiyo huku wengi wakimsuta vikali kwa kuwa nabii wa uongo ilhali anajihusisha na mambo yanayokwenda kinyume na maadili ya kikristo.

Utakumbuka tangu Size 8 atawazwe kuwa kasisi watu wengi wamekuwa wakitilia uwezo wake wa kueneza injili wengi wakihoji kuwa msanii huyo hajatosha kuwa mhubiri kamili kwa kuwa amekuwa akiigiza kuponya wagonjwa na kutoa watu mapepo ilhali ana nyota ya kufanya hivyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke