Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Size 8 ametupasha habari njema kuhusu ujio wa album yake mpya iitwayo Christ Revealed ambayo ana mpango wa kuiachia wikiendi hii.
Kupitia ukurasa wake wa instagram amesema album yake hiyo itaingia sokoni februari 13 mwaka huu ingawa hajaweka wazi wasanii aliowashirikisha na idadi ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya.
Hata hivyo amesema anamshukuru mungu kwa kumwezesha kukamilisha album hiyo ikizingatiwa kuwa safari ya kuandaa album yake hiyo hajakuwa rahisi kutokana na changamoto nyingi alizokutana nazo.
Christ Revealed inakuwa album ya kwanza kwa mtu mzima Size 8 tangu akumbutie ukristo miaka tisa aliyopita baada ya kuachana na muziki wa kidunia.