Nguli wa muziki wa hiphop duniani Snoop Dogg ameikata kiu ya mashabiki zake, kwani tayari ameiweka sokoni Album yake mpya inayokwenda kwa jina la ALGORITHM.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram snoop dogg Amethibitisha hilo kwa kuandika ujumbe unaosomeka ” • ALGORITHM available Now” ikiashirikiana album hiyo tayari inapatika kwenye Digital platforms zote za kupakua na kusikiliza muziki duniani.
ALGORITHM ina jumla ya ngoma 25 ikiwakutanisha wakali kama Usher, BustaRyhmes, Wiz Khalifa na wengine kibao.
“ALGORITHM” ni album ya 19 kwa mtu mzima Snoop Dogg baada ya album yake ya “From Tha Streets 2 Tha Suites” iliyotoka mwezi Aprili mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto.