You are currently viewing SNOOP DOGG ADOKEZA MPANGO WA KUNUNUA MTANDAO WA TWITTER

SNOOP DOGG ADOKEZA MPANGO WA KUNUNUA MTANDAO WA TWITTER

Rappa mkongwe kutoka Marekani Snoop Dogg ameibuka na kutangaza anataka kuununua mtandao wa Twitter

Hii ni baada ya Bilionea Elon Musk kutangaza kwamba dili lake la kuinunua Kampuni ya Twitter imesitishwa kwa muda kufuatia uwepo wa akaunti bandia

Sasa jmbo limemuibua Snoop Dogg kupitia ukurasa wake wa Twitter na ku-tweet yuko tayari kukamilisha ununuzi wa mtandao huo kwa kuandika ujumbe unaosomeka “Huenda watu wawili wakanunua Twitter sasa,” huku akisindikiza na hashtag #WhenSnoopBuysTwitter

Snoop Dogg ameyataja mambo kadhaa ambayo atayafanya kama mmliki mpya wa mtandao huo wenye mamilioni ya wafuasi duniani kote, akiutaja mpango wa kumpa kila mtumiaji wa mtandao huo alama ya bluu iliyothibitishwa (Verification blue checkmark).

“Kila mtu anapata alama ya bluu. hata roboti zenye majina yenye herufi 10 ambazo zinakufuata DM’s na kutoa tu salamu” ameeleza Dogg.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 50, hata hivyo bado haijafahamika kwa undani zaidi ikiwa anadhamira ya dhati ya kuinunua Twitter baada Bilionea Elon Musk kutangaza kusitisha kwa muda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke