You are currently viewing SNOOP DOGG AFUNGULIWA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO

SNOOP DOGG AFUNGULIWA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO

Mkongwe wa muziki wa HipHop kutoka nchini Marekani Snoop Dogg amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono na mwanamke mmoja, kufuatia tukio ambalo lilitokea mwaka 2013.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Mei 29, mwaka wa 2013 mwanamke huyo ambaye hakutaja jina lake amesema alihudhuria moja ya onesho la Snoop Dogg mjini Anaheim, California.

Snoop Dogg alikuwa na swahiba wake aitwaye Bishop Don Juan na walimpatia ‘lift’ mwanamke huyo ambaye hakuwa na usafiri usiku akiwaomba wamfikishe nyumbani kwake. Baada ya kupatwa na usingizi kwenye gari, mwanamke huyo amedai kwamba badala ya kupelekwa kwake, alijikuta asubuhi yupo nyumbani kwa Bishop Don Juan kitandani na alikuwa akitoa Uume wake na kumwekea usoni. Baadaye alimpa nguo ya kuvaa na kuelekea studio kwa Auncle Snoop.

Baada ya kufika studio, mwanamke huyo anasema hali yake ilikuwa sio nzuri, hivyo akaomba aingie chooni, akiwa huko anasema alimuona Snoop Dogg akiingia na kusimama mbele yake akiwa ametoa uume wake nje na kumwekea usoni, kisha alianza kumlazimisha kufanya ngono ya mdomo yaani Oral Sex.

Hata hivyo upande wa mtu mzima Snoop Dogg umejitokeza na kusema kwamba tuhuma hizo hazina ukweli wowote na mwanamke huyo anajitafutia pesa tu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke