You are currently viewing SOCIALITE MAARUFU MTANDAONI VERA SIDIKA KUFANYA TENA UPASUAJI WA MATITI

SOCIALITE MAARUFU MTANDAONI VERA SIDIKA KUFANYA TENA UPASUAJI WA MATITI

Mrembo maarufu mtandaoni nchini Kenya na Afrika Mashariki, Vera Sidika amesema atafanya tena upasuaji wa matiti yake ili kuboresha muonekana wake baada ya kumaliza kuzaa.

Kupitia Instagram page yake Vera Sidika amesema anatamani kupata matiti yenye umbo la mviringo na ambayo yamesisima ila kwa sasa anataka kwanza aikuze familia yake.

“Kunyonyesha hakujawahi kunisumbua hata kidogo, inafanya hivyo kwa kujivunia na nina furaha nyingi. Mara tu baada ya kumaliza kupata watoto, hakika nitafanyiwa upasuaji wa kubadilisha umbo la matiti yawe ya kuvutia, ya mviringo na yaliyoinuka,” amesema Vera.

Ikumbukwe Vera Sidika ambaye miaka michache iliyopita alifanyiwa upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti yake pia ameweka wazi kwamba amekuwa akijivunia sana kumnyonyesha binti yake, Asia Brown.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke