Socialite maarufu nchini Amber Ray amegeukia kufanya muziki ikiwa ni katika kutimiza ndoto zake za kuwa mwiimbaji.
Amber Ray amesema ndoto za kuimba alikuwa nazo kabla ya kuanza kuwa mwanamitindo, hivyo anafurahia kuzikikamilisha kwa sasa.
Amber Ray ambaye ametamba kwenye mitandao ya kijamii kwa miaka mingi ameshirikishwa kwenye wimbo uitwao “Monica” wa msanii Shifuu.
Hata hivyo ngoma hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambao wameonekana kumkatisha tamaa asigeukia muziki kwani hana kipaji cha kuimba huku wengine wakimpongeza kwa hatua ya kuonesha upande wake mwingine kando na ucheshi.
Amber Ray anajiunga kwenye orodha ya mastaa ambao hapo awali walitambulika kama washawishi wakubwa kwenye mitandao ya kijamii na baadae wakageukia kufanya muziki.