You are currently viewing SOL GENERATION YAMSAINI BIEN WA SAUTI SOL

SOL GENERATION YAMSAINI BIEN WA SAUTI SOL

Lebo ya Sol Generation imetangaza kumsaini  msanii Bien Aime Baraza kwa mkataba wa shillingi millioni 50.

Mkataba wa msanii huyo utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu na umekuja wakati huu wasanii wa kundi la Sauti Sol wamezindua mpango wa kuachia kazi zao kama wasanii wa kujitegemea.

Sauti Sol kama kundi  bado limesainiwa kwenye lebo ya Universal Music lakini Bien amejiunga na Sol Generation kama msanii wa kujitegemea.

Bien  anaungana na msanii Bensoul pamoja na Nviiri The Storyteller ambao wamekuwa wakitamba katika tasnia ya muziki  nchini na nyimbo kama, Nairobi na Niko Sawa.

Kusaini kwa Bien kwenye lebo ya sol generation inakuja mra baada ya msanii huyo kuachia EP yake mpya iitwayo Bald Men Love Better, iliyomshirikisha mpiga kinanda maarufu nchini Aaron Rimbui

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke