Rapa wa kike nchini Sosuun amemsuta vikali msanii vivian kwa madai ya kuvumnjia heshima aliposema kwenye moja ya post yake kwenye mtandao wa Instagram kuwa familia ya msanii huyo ndio imeua kipaji chake cha muziki.
Kwenye post hiyo vivian alitoa rai kwa sosuun arudi tena kwenye muziki kutokana na mashabiki kukosa nyimbo zake kwa muda ambapo alienda mbali zaidi kudai kuwa hatua ya sosuun kupotea kwenye muziki imetokana na yeye kujikita zaidi kwenye masuala ya familia, jambo ambalo amedai limemponza kimuziki.
Sasa Kupitia instagram wake Sosuun aliibuka na kutupia maneno mazito vivian kwa kusema kwmbaa aache kumfuatilia maisha yake na badala yake amzalie mume wake watoto aone kama atabaki kwenye muziki wake ambapo amejitapa kwa kusema kwamba amemzidi kimuziki licha ya ukimya wa miaka 10 kwenye muziki wake.
Haikushia hapo Sosuun alienda mbali zadi na kumtaka vivian abadili muonekano wake wa kisanii huku akisema kwamba msanii huyo anajishusha kimuziki kwa kuvalia mavazi yasioendana na brand yake licha ya kuwa mwiimbaji mzuri.
Hata hivyo hatua ya wawili hao kutupiana maneno makali mitandaoni imeonekana kuibua maswali miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ambapo baadhi ya wamemnyoshea kidole cha lawama vivian kwa kumvunjia heshima sosuun kwa kuyaweka mapungufu yake mtandaoni huku wengine wakihoji kuwa huenda wawili hao wanatengeneza mazingira ya kuzungumziwa ili waweze kuachia ngoma ya pamoja.