Rapa kutoka Marekani Soulja Boy amefunguka na kudai kuwa hatokuja kufanya Kolabo na rapa mwenzake Tekashi 69 hadi mwisho wa dunia.
Kwenye mahojiano na Podcast ya Mtangazaji Raquel Harper “It’s Tricky with Raquel Harper” rapa hyo aliulizwa ni namna gani atalipokea ombi la Kolabo kutoka kwa Tekashi 69 ambapo, alijibu kwa kusema kwamba “Haiwezekani, sitakuja kufanya wimbo na wewe (6ix9ine), hatuwezi kufanya wimbo na analijua hilo, hatarajii kupata verse ya Soulja Boy, anafahamu hilo.”
Utakumbuka mwaka wa 2019 kwenye mahojiano na The Breakfast Club, Soulja Boy alisema Tekashi 69 ni zao lake kwani anaamini amemshawishi kuingia kwenye muziki ambapo aliishia kumuita mtoto wake.