Spice Diana ni mmoja wa wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa nchini Uganda.
Kwa miaka mitatu mfululizo, ameshinda kipengele cha msanii bora wa kike wa mwaka katika Tuzo za Zzina lakini pia ameteuliwa kushiriki kwenye Tuzo nyingi za Kimataifa kama vile Afrimma.
Spice Diana pia ni mmoja wa wanamuziki nchini uganda ambao wana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii kwani ana zaidi ya wafuasi milioni moja kwenye mtandao wa Instagram na Facebook mtawalia.
Hitmaker huyo wa “Body” amedai kwamba wafuasi wengi ambao wanamfutilia kwenye mitandao ya kijamii ndio zimempelekea kufanya kolabo za kimataifa ambazo kwa mujibu wake zimetanua wigo wa mashabiki wake.
Ikumbukwe mpaka sasa Spice Diana ameshirikiana na mastaa wakubwa Afrika mashariki kama Harmonize, Zuchu, Mbosso na wengine kibao katika kipindi cha miaka miwili iliyopita