Msanii kutoka nchini Uganda Spice Diana amedai kwamba ugomvi miongoni mwa wasanii haisaidi kuwajenga kisanaa
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema wasanii wanaojihusisha na bifu kwa lengo la kutanua wigo wao kimuziki, wanaharibu brand au chapa zao kwenye jamii.
Hitmaker huyo wa “Boss” amesema kwa sasa ana muda wa kupishana na wasanii wenzake kwani ameamua kuwekeza nguvu zake kujiboresha kisanaa kwa ajili ya kukuza brand yake.
Utakumbuka Spice Diana amekuwa akihusishwa kuwa kwenye ugomvi na wasanii Sheebah Karungi pamoja na Gravity Omutujju jambo ambalo yeye binafsi amekuwa akikanusha kwenye mahojiano mbali mbali.