Msanii wa Source Management, Spice Diana amepuzilia mbali uvumi unasambaa mtandaoni kwamba hakuwaalika baadhi ya wasanii kwenye uzinduzi wa EP yake mpya Star Gal.
Katika mahojiano yake hivi karibuni amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa alituma mwaaliko kwa kila msanii kupitia uongozi wake.
Mkali huyo wa ngoma ya “Tujooge” amesema hana ugomvi wowote na msanii yeyote nchini uganda na kama kuna msanii hakupokea barua ya mwaaliko, uongozi wake ndio wakulaumiwa kwa kutomfikishia ujumbe.
Kauli ya Spice diana imekuja mara baada ya wasanii Gravity Omutujju na Lydia Jazmine kudai kuwa hawakupata mwaaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa EP mpya ya Spice Diana