You are currently viewing SPICE DIANA AMJIBU GRAVITY OMUTUJJU KITAALAM

SPICE DIANA AMJIBU GRAVITY OMUTUJJU KITAALAM

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Spice Diana amemjibu rapa Gravity Omutujju kisomi baada ya rapa huyo kumshambulia kwa kudai kwamba ni mnafiki.

Katika mahojiano yake Spice Diana amesema hana muda wa kupishana na Gravity Omutuju kwa kuwa ameelekeza nguvu zake zote kutangaza muziki wake ili uwafikie watu wengi duniani.

Mwishoni mwa juma lilopita Gravity Omutujju alimshambulia Spice diana na meneja wake akidai kwamba wawili hao wana roho mbaya kwani hawajawahi watakia wasanii wengine mema.

Gravity Omutujju alitoa kauli hiyo  baada ya spice diana kuwaalika wasanii wengi kwenye hafla ya uzinduzi wa EP yake mpya iitwayo Star Gal.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke