Mwanamuziki kutoka Uganda Spice Diana amedai kuwa hataruhusu wasanii watakaovalia mavazi yanayokwenda kinyume na madili ya jamii kutumbuiza kwenye tamasha lake la muziki mwaka 2023.
Katika mkao na wanahabari Spice Diana amesema tamasha hilo itakuwa ya kifamilia zaidi, hivyo kutakuwa na ustaarabu kwenye suala la mavazi.
Mrembo huyo amesema tayari ana timu ya watu ambao watakagua wasanii watakaokuwa wanatoa burudani jukwaani kama njia moja wapo ya kuzuia wasanii watakaovalia mavazi yasiokuwa na heshima.
Spice Diana anatarajiwa kufanya onesho lake Januari 13 mwaka 2023 huko Cricket Oval, Lugogo na itakuwa mara yake ya kwanza kufanya shoo kwenye ukumbi huo mkubwa zaidi nchini Uganda tangu aanze safari yake ya muziki.