You are currently viewing SPICE DIANA ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA TUZO UGANDA KUWAPA WASANII PESA

SPICE DIANA ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA TUZO UGANDA KUWAPA WASANII PESA

Msanii nyota nchini Uganda Spice Diana amewataka waandaji wa tuzo nchini humo kuanza kuwapa wasanii pesa badala ya tuzo pekee.

Akizungumza alipopokea tuzo ya msanii bora wa mwaka kutoka kwa kampuni ya MTN Uganda Spice diana amesema pesa inawafanya wasanii wajihisi vizuri zaidi ikizingatiwa wengi wao wamewekeza pesa nyingi kwenye kazi zao za muziki.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mbikka” ametoa changamoto kwa waandaji wengine wa tuzo kufuata nyayo za MTN za kutambua juhudi za wasanii kwa kuwapa pesa pamoja na tuzo mtawalia.

Kauli ya Spice diana imekuja mara baada ya kutunikiwa shillingi millioni 3 za Uganda kusindikiza tuzo ya msanii bora wa mwaka aliyopewa na kampuni MTM kupitia Callers Tune Awards.

Utakumbuka kampuni ya mawasiliano ya MTN Uganda wikiendi hii iliyopita iliwazawadi tuzo  wasanii wote ambao nyimbo zao zilipakuliwa zaidi kama caller tunes kwa mwaka wa 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke