Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Spice Diana amekuwa akikana kuwa kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi na meneja wake, Roger Lubega.
Katika mahojiano ya hivi karibuni mrembo huyo amewaacha mashabiki zake na maswali mengi kama kweli anatoka kimapenzi na meneja wake au la.
Hii ni baada ya Spice Diana kusikika akisema kwamba kwa sasa hawapo kwenye uhusiano wa kimapenzi ila meneja wake Roger Lubega akimchumbia hawezi kataa.
Jibu ya hitmaker huyo wa “Body” imewaaminisha mashabiki kuwa kuna jambo linaendelea kati yake na meneja wake Roger Lubega huku wakiwa na matumaini huenda hivi karibuni wawili hao wakaweka wazi mahusiano ya kimapenzi.
Miezi michache iliyopita katika siku ya kuzaliwa kwa meneja wake, Spice Diana alisema kwamba angeweza kufikia hapa alipo bila uwepo wa Roger Lubega ambaye amempambania sana kwenye muziki wake.