Staa wa muziki nchini Uganda Spice Diana amewatolea uvivu watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaodai muziki wake ni takataka.
Kupitia video aliyochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii Spice Diana amesema ana mashabiki wengi wa muziki Afrika mashariki ambao wanapenda muziki wake, hivyo hatatishwa na watu wachache ambao wamelipwa kumharibia jina.
Hitmaker huyo wa “Upendo” amesema hatua yake ya kukosoa tuzo za Janzi haikuwa kwa sababu hakushinda chochote kwenye tuzo hizo ila alikuwa anataka uwazi.
Hata hivyo amesema baadhi ya tuzo huandaliwa kwa ajili ya kuwashusha kimuziki baadhi ya wasanii na baadae kuwaita feki.
Kauli ya Spice Diana imekuja mara baada ya kuwatupia lawama waandaji wa tuzo za Janzi kwa kusema kwamba ni wala rushwa, tuzo ambazo zilifinyika wikiendi hii iliyopita kwa mara ya kwanza chini Uganda.