You are currently viewing Spice Diana awajibu wanaoshinikiza aingie kwenye ndoa

Spice Diana awajibu wanaoshinikiza aingie kwenye ndoa

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Spice Diana amedai kwamba hana mpango wa kuingia kwenye ndoa hivi karibuni.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema ana mambo mengi ya kutimiza kabla ya ndoa.

Mrembo huyo ambaye hajawahi kumtambulisha mpenzi wake kwa umma, anaamini ndoa ni jambo zuri lakini inapaswa kufanywa kwa wakati sahihi.

Hata hivyo amewataka mashabiki zake kuacha kumpa shinikizo zisizo kuwa na msingi na badala yake waendelee kufuatilia kazi zake.

“Nitafunga ndoa tu wakati muafaka ukifika. Nina mengi ya kutimiza kabla ya ndoa. Mashabiki zangu wanapaswa kunidai muziki, sihamasishi watu kupitia ndoa,” Alisema.

Ikumbukwe Spice Diana kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya tamasha lake ambalo lifanyika Januari 13 mwaka 2023 katika uwanja wa Cricket Oval, Lugogo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke