Mwanamuziki kutoka Uganda Spice Diana ameonesha kusikitishwa na hatua ya promota Robert Mutima kukataa kumlipa pesa zake zilizosalia baada ya kutumbuiza kwenye show ya promota huyo huko Masaka.
Mrembo huyo amesema licha ya promota huyo kuahidi kumlipa pesa hizo kwa wakati hadi sasa hajatimiza ahadi yake hiyo ambapo amehapa kuwa ataendelea na harakati ya kumshinikiza amlipe haki yake.
Utakumbuka mwezi uliopita Spice Diana alikamata vichwa vya habari nchini Uganda alipomkashifu Mutima hadharani akiwa jukwaani baada ya kushindwa kulipa pesa zake, lakini wawili hao walikuja wakakutana ambapo promota huyo aliomba radhi na kuahidi kumlipa.