You are currently viewing SPICE DIANA AZIPONDA TUZO ZA JANZI AWARDS 2021 KISA UPENDELEO

SPICE DIANA AZIPONDA TUZO ZA JANZI AWARDS 2021 KISA UPENDELEO

Mkali wa muziki kutoka Spice Diana ni muhanga wa tuzo mpya za Janzi Awards, ameibuka na kuwatupia lawama kwamba ni wala rushwa.

Licha ya kuachia ngoma kali mwaka huu mrembo huyo alishindwa kuibuka na tuzo ya msanii bora wa mwaka kwenye tuzo za Janzi Awards 2021 ambazo zilifanya kwa mara ya kwanza katika Bustani ya Kololo Independence nchini Uganda.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Spice Diana amewashutumu waandaji wa tuzo za Janzi kwa kashfa za rushwa na kuomba uwazi katika uteuzi.

Hitmaker huyo wa “Upendo” amesema ameshindwa ni njia ipi waandaji wa tuzo za Janzi walitumia kumpata msanii aliyeshinda kipengele cha msanii bora wa mwaka.

Spice Diana alikuwa akichuana na wasanii wengine wa kike kama Azawi, Winnie Nwagi, Rema Namakula, Nina Roz, Cindy Sanyu, Shebah Karungi lakini tuzo ya msanii bora wa kike kwenye tuzo za Janzi Awards mwaka wa 2021 zilimuendea Azawi.

Ikumbukwe zaidi ya wasanii 300 waliteuliwa kushiriki kwenye tuzo za Janzi kwa mwaka wa 2021 ambapo kura 75,000 zilipigwa kwenye tuzo hizo ambazo ziliandaliwa kwa ajili ya kutambua mchango na kutoa heshima kwa wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke