You are currently viewing SPICE DIANA MBIONI KUANDAA ONESHO LAKE LA MUZIKI

SPICE DIANA MBIONI KUANDAA ONESHO LAKE LA MUZIKI

Msanii Spice Diana ameripotiwa kuwa yupo mbioni kuja na onesho lake la muziki huko Cricket Oval viungani mwa jiji la Kampala.

Chanzo cha karibu na msanii huyo wa Source management kimesema Spice Diana anatarajiwa kufanya onesho lake la muziki katika ukumbu wa Cricket Oval mwakani.

Inadaiwa Spice Diana anataka kuweka rekodi ya kujaza ukumbi huo ambao hujaza zaidi ya watu 20, 000 ikizingatiwa kuwa amekuwa akifanyia shows zake kwenye ukumbi wa Freedom City ambao ni mdogo ikilinganishwa na Cricket oval.

Utakumba Cricket Oval ni moja kati ya makumbi makubwa ya matamasha nchini uganda na imekuwa ikitumika na mastaa makubwa nchini humo kufanya maonesho yao.

Chameolene alikuwa msanii wa kwanza kujaza ukumbi huo na tangu wakati huo wasanii wengine walifuata mkumbo huo akiwemo Gravitty omutujju na Levixone ambao wa pia waliweka historia ya aina yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke