You are currently viewing SPOTIFY IMEONDOA MFUMO WA SHUFFLE PLAY KATIKA ALBUM.

SPOTIFY IMEONDOA MFUMO WA SHUFFLE PLAY KATIKA ALBUM.

Adele ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakipinga Streaming Platforms zinavyolazimisha kuweka button ya “Shuffle” ambayo inapiga nyimbo kuendana na Algorithm inavyopanga na sio kama nyimbo zinavyojipanga katika Album.

Spotify imekubali maombi ya Adele na imetoa alama ya “Shuffle” katika button ya “Play”. Sasa hivi ukibonyesha button ya “Play” katika album yoyote utaweza kusikiliza nyimbo kama zilivyojipanga katika Album. Kama utahitaji Shufle Play itakwepo katika sehemu ya Now Playing na sio katika Album.

Hakuna jambo linatokea kwa bahati mbaya, pia inawezekana ilikuwa ni plan ya Spotify kuondoa Shuffle katika Albums, so imeamua kwenda na kiki ya Adele ili kuonekana inajali na kusikiliza wasanii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke