You are currently viewing SQUID GAME YAWEKA REKODI EMMY AWARDS 2022

SQUID GAME YAWEKA REKODI EMMY AWARDS 2022

Ikiwa ni msimu wa 74 wa kutoa tuzo za Emmy Awards 2022, orodha za majina ya wanaowania yatajwa.

Sasa series maarufu ya “Squid Game” kutoka Korea Kusini imeweza kuweka rekodi kwenye tuzo hizo. Imetajwa kuwania tuzo 14 za Emmy. Rekodi hii inaifanya kuwa series ya kwanza isiyotumia lugha ya Kiingereza kuwania idadi hiyo ya tuzo.

Squid Game imezipiku series nyingine kali kama, “Better Call Saul,” “Euphoria,” “Ozark,” “Severance,” “Stranger Things,” “Succession,” na “Yellowjackets.”

Aidha, waigizaji nyota watano wa “Squid Game” wameteuliwa kuwania kwenye vipengele mbalimbali na kuwafanya waigizaji wa kwanza wa Korea katika historia kupata uteuzi katika vipingele vyao.

Hafla ya ugawaji wa tuzo za Emmy mwaka huu inatarajiwa kufanyika Septemba 12, katika ukumbi wa Microsoft Theater jijini Los Angeles, pia matukio yote yataruka mubashara kupitia NBS.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke