You are currently viewing SSARU AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA TRIO MIO

SSARU AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA TRIO MIO

Female rapper kutoka Kenya Sylvia Ssaru ameibuka na kukanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na msanii mwenzake Trio Mio.

Hii ni baada ya wawili hao kuonekana kuwa na ukaribu katika siku za hivi karibuni toka walipoachia ngoma ya pamoja iitwao “Kichwa tu” ambayo wamemshirikisha Timmy Tdat.

Akijibu swali la shabiki yake aliyetaka kujua kama kweli ana uhusiano wa kimapenzi na Trio Mio kwenye mtandao wa instagram Ssaru amesema hakuna kitu chochote kinaendelea kati yake na trio mio huku akidai kuwa uhusiano wao utabaki kuwa wa ndugu na dada.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumshambulia Ssaru ambapo wengi wamedai kuwa mrembo huyo ambaye ni mkubwa kiumri ana mpango wa kumharibu kimaadili Trio Mio ambaye bado anasoma shule ya upili.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke