Mafanikio ya wimbo wa ‘Toto’ yanaonekana yanampa Staa wa muziki nchini Willy Paul jeuri ya kufikiria kuachia wimbo mwingine mpya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul amewaachia mashabiki zake swali iwapo aachie wimbo mpya mara baada ya wimbo wake wa Toto kufikisha zaidi ya views millioni moja kwenye mtandao wa youtube.
Hata hivyo mashabiki zake wameonekana kuitikia wito wake wa kuachia wimbo mpya, hivyo huenda mtu mzima Willy Paul akawabariki na singo mpya muda wowote kuanzia sasa.
Utakumbuka Toto ni wimbo unaopatikana kwenye album yake ya pili African Experience ambayo pia inafanya poa kwenye mtandao wa Boomplay Kenya ikizingatiwa kuwa mpaka sasa ina zaidi ya streams millioni moja.