Upendo wa Staa wa muziki nchini Bahati kwa baby mama wake Diana B unazidi kuongezeka kila uchao.
Baada ya kumnunulia gari aina Prado TX kama zawadi ya siku ya wapendanao duniani amekuja na suprise nyingine kwa mke wake huyo.
Kupitia ukurasa wake wa instagram hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amepost mjengo wa kifahari ambao amezawadi mke wake Diana B na kusema kwamba ameahamua kumpa zawadi hiyo kama njia ya kumuonyesha upendo kwa kusimama nae kwenye shida na raha.
Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wameonekana kufurahishwa na hatua ya Bahati kumuonyesha upendo baby mama wake huku wakimpongeza kwa mafanikio makubwa maishani.