Album mpya ya rapa Stamina iitwayo PARADISO imetoka rasmi na sasa inapatikana exclusive kupitia BoomPlay.
Album hiyo ina jumla ya nyimbo 13, huku wasanii kama Kayumba, Isha Mashauzi, Saraphina, Linah, Aslay, Walter Chilambo na wengine wengi wakisikika kwenye kolabo mbalimbali ndani ya album hiyo.
“Paradiso” inakuwa album ya pili kwa mtu mzima Stamina tangu aanze safari yake ya muziki baada ya “Mlima Uluguru” ambayo ilitoka mwaka wa 2015.