Mwanamuziki kutoka Uingereza ambaye ni mpenzi wa msanii kutoka Nigeria Burna Boy, Stefflon Don amechukizwa na hatua ya Burna Boy kujitangaza kuwa hana mpenzi kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Burna Boy aliandika ujumbe unaosomeka “Kwa taarifa yako, Odogwu hana mke.”
Kauli hiyo ambayo iliamsha majibu ya wawili hao kuwa tayari wameachana, ilimuibua Stefflon Don ambaye alimrushia dongo Burna Boy kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema “Umaarufu na pesa hubadilisha baadhi ya watu”
Mwimbaji huyo wa Uingereza alienda mbali zaidi na kusema, haijalishi ni kwa kiasi gani umemuonesha mtu upendo, uaminifu na vile umemfanyia mazuri, watu hujifanya wema kumbe ni feki tu.
Stefflon Don na Burna Boy wameachana baada ya kuwa penzini kwa miaka mitatu.