Mwimbaji Stefflon Don anaamini Burna Boy alimuimba kwenye wimbo wake maarufu “Last Last” ambao ulitoka Mei mwaka huu.
Kwenye mahojiano na TT Torrez, Stefflon amesema alikuwa penzini na Burna Boy kwa miaka miwili na nusu na tangu wameachana mwaka mmoja uliopita hajaingia tena kwenye mahusiano mapya.
Licha ya Stefflon Don kukubali kuwa Burna Boy alimlenga kwenye wimbo huo, amepingana na baadhi ya mistari kwa kusema mingine ambayo ameyazungumza Burna kwenye ngoma hiyo hayana ukweli.