You are currently viewing STEPHEN KASOLO AWAOMBA MSAMAHA MASHABIKI KWA KITENDO CHA KUMTISHIA KUMUUA BINTI YAKE

STEPHEN KASOLO AWAOMBA MSAMAHA MASHABIKI KWA KITENDO CHA KUMTISHIA KUMUUA BINTI YAKE

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Stephen Kasolo amelazimika kuomba radhi mashabiki zake mara baada ya kumtisha kumuua binti yake wa miaka mitatu kwenye moja ya video iliyosambaa mitandaoni kwa madai ya kuvunja chupa ya maji ya bei ghali.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Kasolo amewataka mashabiki zake wamsamehe kwa hatua ya kumdhalalisha binti yake huku akihapa kutorudia kitendo cha kumfokea mtoto wake kwa hasira ikizingatiwa kuwa hakukusudia kumtishia binti yake kama ilivyotafsiri kwenye mitandao ya kijamii.

Kauli ya Kasolo imekuja mara baada ya wakenya kumshushia kila aina ya matusi kwa hatua ya kumtishia maisha mtoto wake ambapo walienda mbali zaidi na kudai kuwa msanii huyo hana kabisa vigezo vya kuwa mzazi.

Purukushani hiyo ilikuja kufuatia video ya Kasolo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo alisikika akimfokea binti yake kwa hasira huku akimtolea vitisho ya kumtoa uhai kwa madai ya kuivunja chupa ya maji ambayo kwa mujibu wake ni ya bei ghali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke