You are currently viewing STEVE NYERERE: SITOJIUZULU KAMA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

STEVE NYERERE: SITOJIUZULU KAMA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania Steve Nyerere amedai kwamba hatojiuzulu kwenye wadhfa wake licha ya shinikizo anazozipokea kutoka kwa baadhi ya wasanii.

Akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Nyerere amesema uteuzi wake ukitenguliwa atakata rufaa mahakamani huku akisisitiza kuwa ana nia njema ya kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Bongofleva.

“Sijiuzulu na wala sitoki, nina nia ya kuendeleza industry ya nchi hii.” Amesema Steve Nyerere

Ikumbukwe juzi kati wakati kamati la Shirikisho la muziki Tanzania lilimteua Steve Nyerere kuwa msemaji wa shirikisho hilo, wadau wengi wa sanaa nchini Tanzania walipinga vikali uteuzi wake wakidai kuwa hana vigezo kabisa vya kuwasimamia wanamuziki.

Hata hivyo Mwenyekiti wa shirikisho la wasanii Tanzania Rapa Fid Q alipokea maoni ya waliopinga uteuzi wa Steve Nyerere kwa mikono miwili ambapo alienda mbali zaidi na kutangaza mkutano utakaowaleta pamoja wadau mbali mbali wa sanaa, Machi 21, 2022 kujadili mustakabali wa shirikisho hilo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke