Msanii Stivo Simple Boy amefunga ndoa ya kitamudani maarufu kama Ruracio na mchumba wake Jenny Wangui ikiwa ni miezi kadhaa tangu amvishe pete ya uchumba.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Stivo ameposti ujumbe mrefu wa mahaba kwa mrembo huyo na kusema kwamba amechukua maamuzi hayo kama njia ya kuwathibitishia wazazi wa Jenny Wangui kuwa hafanyi mzaha katika mahusiano yake bali ameamua kwa kauli moja kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Hitmaker huyo “Freshi Barida” ambaye amepongezwa na mashabiki zake kwa hatua hiyo kubwa maishani, amemuondolea hofu mpenzi wake kwa kumueleza kuwa penzi lake ni la kweli, hivyo asitishwe na watu mitandaoni.
Hii ni baada ya mwanamke mmoja kujitokeza na kudai kuwa amemzia kimapenzi Stivo the Simple Boy, kitendo kilichomfanya gee kuwa na wasi wasi juu ya hatma ya mahusiano yake na msanii huyo wa Men in Business.