You are currently viewing STEVO SIMPLE BOY AMTOLEA UVIVU EX WAKE PRITTY VISHY KISA MAHARI YA SHILLINGI MILLIONI 2

STEVO SIMPLE BOY AMTOLEA UVIVU EX WAKE PRITTY VISHY KISA MAHARI YA SHILLINGI MILLIONI 2

Msanii Stevo Simple Boy amepuzilia mbali mahari ya shillingi millioni 2 ambayo mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy aliweka wazi kwa wanaume wanaotaka kumchumbia.

Katika mahojiano na mpasho Stevo amesema mrembo huyo anatumia suala kutafuta mazingira ya kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii  kwani dhamani yake haiendani na kiwango cha mahari alichodai.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Freshi Barida” ameweka wazi sababu zilizompelekea kuachana na Vishy kwa kusema kwamba mrembo huyo alimsaliti kimapenzi kwa kutoka kimapenzi na wanaume wengine.

Hata hivyo amekanusha madai ya Pritty Vishy kuwa amekuwa akimlilia warudiane kwa kusema kwamba  penzi lao lilivunja kitambo na hawezi kumrudia kutokana na tabia zake ambazo hazikumfurahisha hata kidogo.

Mbali na hayo msanii huyo ambaye chini ya lebo ya muziki ya Men in Business amedokeza ujio wa tamasha lake la Freshi Barida ambalo linalenga kukuza vipaji vya vijana chini.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke