Stevo Simple Boy avunja kimya chake baada ya kufiwa na baba yake mzazi

Msanii kutoka nchini Kenya Stevo Simple Boy amevunja ukimya wake siku chache baada ya kufiwa na Baba yake mzazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wamekuwa wakimuonyesha kwenye muziki huku akitoa wito wamweka kwa maombi wakati huu mgumu familia yake inaomboleza kuondokewa kwa mpendwa wao.

“Nashukuru Sana mashabiki kwa kunisapoti huu wakati wote ila nimepata msiba wa kupoteza Babangu mzazi naomba mniombee na mnipee nguvu wakati huu”, Aliandika.

Kauli ya Stevo imekuja mara baada ya kufanikiwa kurejesha umiliki wa akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram ambayo imekuwa mikononi mwa wadukuzi kwa wiki kadhaa sasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke