You are currently viewing STEVO THE SIMPLE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

STEVO THE SIMPLE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

Msanii Stevo the Simple Boy hataki kupoa kabisa kwenye suala la kuupeleka muziki wake kimataifa, hii ni baada ya kutangaza ujio wa tamasha lake la muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Iinstagram Stevo amesema tamasha lake litaitwa freshi barida huku akiwaachia mashabiki swali kama watanunua tiketi za tamasha hilo ambalo anajianda kuja na nayo hivi karibuni.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ni Nani” amesema anaenda kuweka historian nchini na afrika kwa ujumla kupitia freshi barida concert huku akiwataka mashabiki zake wapendekeze wasanii wao pendwa ambao wangependa awajumuishe kwenye tamasha lake hilo.

“TULIONA SHINCITY NASASA TUTAONA FRESHI BARIDA CONCERT… HISTORIA ITAONEKANA NCHINI KENYA NA AFRICA MZIMA… JE UTANUNUA TIKITI? NA UNATAKA KUWAONA WASANI WAGANI KWENYE CONCERT YANGU?”, Ameandika kupitia Instagram yake..

Kauli ya Stevo imekuja mara baada ya kuachia wimbo wake mpya uitwao freshi barida siku kadhaa baada ya kutasanua kuwa anakuja na kinywaji chake kiitwacho freshi barida energy.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke