You are currently viewing STEVO THE SIMPLE BOY AZINDUA CHAPA YAKE YA MAVAZI

STEVO THE SIMPLE BOY AZINDUA CHAPA YAKE YA MAVAZI

Msanii Stevo The Simple amezindua chapa yake ya mavazi inayokwenda kwa jina la Freshi Barida.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Stevo amethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba ameamua kuja na chapa ya mavazi ya Freshi Barida kama njia ya kujipatia kipato cha kujiendeleza nayo kimaisha kando na muziki.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mihadarati” amesema chapa hiyo itajishughulisha na masuala ya kuuza kofi, tisheti na hoodie zake zilizoandikwa neno freshi barida ambayo amekuwa akitumia kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni.

Hata hivyo ametoa wito kwa wakenya kumuunga mkono kwenye shughuli yake hiyo ikizangatiwa kuwa anauza kofia pamoja na Tisheti kwa bei ya reja reja ya shillingi 1,000 huku hoodies akiziuza kwa bei ya shillingi 2,500.

Kauli ya Stevo ambaye yupo chini lebo ya muziki ya Men in Business imekuja mara baada ya kudokeza kwamba ana mpango wa kuja na kinywaji chake kiitwacho Freshi Barida Energy Drink kwenye moja ya post yake kwenye mtandao wa Instagram ambayo alikuja baadae akaifuta.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke