You are currently viewing STEVO THE SIMPLE BOY MBIONI KUZINDUA ENERGY DRINK YAKE

STEVO THE SIMPLE BOY MBIONI KUZINDUA ENERGY DRINK YAKE

Inaonekana Msanii Stevo The Simple anataka kugeuza muziki wake kuwa biashara mara baada ya kutangaza  ujio wa kinywaji chake kiitwacho ”Freshi Barida”

Msanii huyo amethibitisha taarifa hiyo njema kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram kwa kuachia mashabiki zake swali kama watauunga mkono atakapoingiza bidhaa hizo sokoni.

Stevo the Simple ni moja ya wasanii chipukizi katika tasnia ya muziki nchini Kenya jitihada zake na uwezo wake umekuwa ukionekana kupitia kazi mbalimbali anazozifanya, kama msanii anayechipukia, hii ni moja ya hatua kubwa katika muziki.

Utakumbuka Stevo ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Men in business amekuwa akitangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni Aprili 28 mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke