Msaniii Stivo Simple Boy ametupasha tusiyoyajua kuhusu maisha yake.
Katika mahojiano na Obinna tv Stivo amesema kuna kipindi alitupwa jela kwa wiki moja baada ya mrembo mmoja kumsingizia tuhuma za ubakaji.
Hitmaker huyo wa ‘Freshi Barida” amesema purukushani kati yake na mrembo ilianza kipindi alipomkata kimapenzi jambo lilimfanya akamshataki kwa mama yake mzazi kuwa alimbaka na hapo ndipo akajipata jela.
Hata hivyo amesema kesi yao ilipokuwa ikiendelea alipelekwa na mrembo huyo hospitali ambapo walifanyiwa vipimo lakini walipotoa matokea ilibainika kwamba madai ya kumbaka mrembo huyo hayakuwa na ukweli wowote, hivyo akaachiwa huru.