You are currently viewing STIVO SIMPLE BOY AFUNGUKA MAOVU YA EX WAKE  PRITTY VISHY

STIVO SIMPLE BOY AFUNGUKA MAOVU YA EX WAKE PRITTY VISHY

Msanii Stivo Simple Boy ameingia kwenye headlines mara baada ya kuanika hadharani maovu ya mpenzi wake wa zamani Prity Vishy.

Akipiga stori na podcast ya Oga Obinna Stivo ameibuka na kudai kuwa Pritty alikuwa na zaidi ya wanaume 50 ambao alikuwa anatoka nao kimapenzi.

Msanii huyo wa Men in Business amesema alikuwa tayari kufunga ndoa na Pritty Vishy lakini mrembo huyo alidinda kubadili mienendo yake ya kutembea wanaume mbali mbali, jambo ambalo anadai lilimpelekea kuvunja uhusiano wake na mrembo huyo.

“Mimi nilikuwa namuambia kama ananipenda ukweli, awachane na hizi vitu zake na akuwe na mtu mmoja tufunge ndoa lakini hakuwa anaelewa.”, Amesema Stivo.

Kauli ya hitmaker huyo wa ngoma ya “Freshi Barida” imekuja mara ya Ex wake Pritty Vish kudai kuwa alimsaliti kimapenzi Stivo Simple Boy kwa kutoka kimapenzi na wanaume wengine ambapo alienda mbali zaidi na kukiri kuwa alikuwa kwenye mahusiano na msanii huyo kwa ajili ya kupoteza muda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke