You are currently viewing Stivo Simple Boy akiri kuchumbiwa na wanawake wenye umri mkubwa

Stivo Simple Boy akiri kuchumbiwa na wanawake wenye umri mkubwa

Msanii Stivo Simple Boy amefunguka usiyoyajua kuhusu maisha yake kwa kusema kuwa wanawake wenye umri mkubwa wamekuwa wakimzimia kimapenzi kupitia mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na Mwende Macharia msanii huyo wa Men in Business amesema wanawake hao wamekuwa wakimuahidi maisha mazuri huku wakimsisitizia kwamba hawatokuja kumkimbia ikitokea ameridhia ombi la kuingia nao kwenye mahusiono.

Hitmaker huyo “Freshi Barida” amesema kwamba hayuko tayari kutoka kimapenzi na wanawake waliomzidi umri kwa sababu watamkimbia akifilisika kiuchumi.

“Wana pesa ndio maana wanadhani nitakubali kutoka nao kimapenzi. Sitaki kujihusisha nao kwa sababu watanikimbia nikifilisika.”, Alisema.

Simple Boy hajakuwa kwenye mahusiano yeyote ya kimapenzi tangu alipoachana na mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy kwa madai ya usaliti.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke