You are currently viewing STIVO SIMPLE BOY MBIONI KUFUNGA NDOA

STIVO SIMPLE BOY MBIONI KUFUNGA NDOA

Msanii wa msanii wa muziki nchini Stivo Simple Boy huenda akafunga ndoa hivi karibuni mara baada ya kuweka wazi mipango yake ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi wake.

Licha ya kutomtaja muhusika, Stivo ameeleza kuwa mpenzi wake huyo ameridhia suala hilo kwani naye pia alikuwa akilihitaji toka mwanzo.

Katika mahojiano na Mungai Eve ameongeza kuwa katika mahusiano amejifunza kunyamaza bila kuyaweka hadharani na wiki ijayo ndipo anatarajia kumtambulisha nyumbani kwao, Mombasani na taratibu nyingine kama kufunga harusi kufuata.

Lakini pia Hitmaker huyo wa Freshi Barida amemtakia kila la heri aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy ambaye juzi kati alijitokeza hadharani na kutangaza kwamba yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii Madini Classic.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke