Meneja wa msanii stivo the simple anayefamika kama Oyo ametuhumiwa kumtumia vibaya msanii huyo.
Kulingana na chanzo cha karibu na Stivo the Simple Boy meneja wake huyo amekuwa akipora pesa za show zote ambazo msanii huyo amekuwa akizifanya, akitoa mfano kuwa Stivo the Simple Boy amekuwa akilipwa Elfu 70 kwa show moja lakini cha kushangaza uongozi wake unamlipia shillingi elfu 2.
Chanzo hicho kimeenda mbali zaidi na kusema kwamba uongozi wa Stivo the Simple Boy umekuwa ukimzuia msanii huyo asitangamane na watu kwa hofu kuwa msanii huyo huenda akaanika madhila anayoyapitia kwenye lebo ya muziki ya Made in Kibera.
Hata hivyo inadaiwa kwa sasa msanii huyo anaishi maisha ya uchochole licha ya kupata dili mbali mbali ambazo zimekuwa zikimuingizia pesa nyingi.
Uongozi wake hata hivyo haujatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoibuliwa na wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii.