Msanii Stivo The Simple amelazimika kufungua akaunti mpya za mitandao ya kijamii baada ya uongozi wake wa zamani kudinda kumpa haki ya kutumia akaunti zake za awali hadi pale atakapowalipa pesa.
Kupitia ukurasa wake mpya wa Instagram Stivo The Simple the Boy ametoa rai kwa mashabiki zake wamfuatilie kwenye akaunti zake mpya ya mitandao ya kijamii kutokana na mzozo ulioibuka kati yake na menejimenti iliyokuwa ikisimamia kazi zake za muziki ya Made In Kibera.
WAKENYA NA MAFANS WANGU NAOMBA SUPPORT YENU🙏 YA DUNIYA NI MENGI, FOLLOW ACCOUNT YANGU MUPYA @stevosimpleboy8 NITASHUKURU SANA 🙏🙏 NDIO MAANAKE..Ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kauli ya Stivo The Simple imekuja miezi kadhaa baada ya uvumi kusambaa mtandaoni kuwa msanii huyo amekuwa akiishi maisha ya uchochole mtaani kufuatia hatua ya meneja wake kufuja pesa zake zote alizositolea jasho, madai ambayo meneja wake huyo alikuja akakanusha kwa kusema kuwa hayana msingi wowote.