Hitmaker wa “Mihadarati” msanii Stivo the Simple amekanusha tuhuma za kunyanyaswa na uongozi wake.
Akiwa kwenye mahojiano na SPM BUZZ Stivo the Simple Boy amesema madai hayo hayana ukweli wowote bali ni taarifa ambayo iliibuliwa na baadhi ya watu wanaotaka kutumia jina lake kujitafutia makuu.
Msanii huyo amesema ana uhusiano uzuri na meneja wake na hajaporwa miraba ya nyimbo zake kama inavyodaiwa mitandaoni.
Hata hivyo Meneja wake anayefahamika kama Oyoo amekanusha tuhuma za kumnyanyasa msanii huyo kwa kusema kwamba madai hayo yaliibuliwa na baadhi ya watu wanaomuonea wivu stivo the simpo boy kutokana na mafanikio ambayo ameyapata kwenye muziki wake.
Ikumbukwe juzi kati chanzo cha karibu na Stivo the Simple Boy kilidai kuwa meneja wake amekuwa akipora pesa zote za show ambazo msanii huyo amekuwa akizifanya, ikitoa mfano kuwa Stivo the Simple Boy amekuwa akilipwa Elfu 70 kwa show moja lakini cha kushangaza uongozi wake umekuwa ukimlipia shillingi elfu 2.
Chanzo hicho kilieenda mbali zaidi na kusema kwamba uongozi wa Stivo the Simple Boy umekuwa ukimzuia msanii huyo asitangamane na watu kwa hofu kuwa msanii huyo huenda akaanika madhila anayoyapitia kwenye lebo ya muziki ya Made in Kibera.